Tuesday, December 22, 2009
Wednesday, May 20, 2009
Monday, April 27, 2009

Fahari yetu katika pitapita zake mitaani mwishoni mwa wiki ilivinjari Bagamoyo kusherehekea sikukuu ya muungano,ambayo kwa bahati mbaya mvua "ilivunja" muungano baada ya kumzuia rais wa Zanzibar mh. Dk. Karume kuudhuria sherehe hizo. Mvua hizo hazikuzuia mapumziko yetu ya sikukuu ampao tulijumuika na wananchi wengine,japo si wengi kutembelea mji ambao ni fahari yetu wa Bagamoyo, na kukuta mjasiliamali mmoja ambaye kwa sababu sikufanikiwa kuongea nae sitoweza kutaja jina ila nilipata fursa ya kupiga picha mojawapo ya vivutio vyake ambavyo vilinifanya nifurahie siku yangu na kujisikia furaha kuona kumbe kuna watanzania ambao ni wabunifu sana katika kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya Taifa letu kwani mbali na kuwaonesha watu fahari yetu hii,pia mjasiliamali huyu huuza mazao ya viumbe hawa nchi za nje na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.
HONGERA MDAU
Saturday, April 25, 2009
Kikwazo ni nini hasa?
Wadau ninaomba kuwakilisha mada ifuatayo, ambayo ningehitaji majibu toka kwenu. Ujasiria mali unaathiriwa vipi na kodi za nchi yetu? Je serikali ifanye juhudi gani kutusaidia sisi wananchi hasa wa kipato cha chini?
Pia naomba nigusie suala la kodi kwa wafanyakazi
Mfanyakazi hasa wale wnaofanya sekta binafsi pindi wapatapo ka bonasi (sijui neno rasmi la kiswahili) basi serikali huchukua asilimia 30 ya hela yake je ni haki kwa serikali kuvuna kiasi chote hicho huku ikiwa haitoi huduma kwa jamii inavyostahili?
Pia naomba nigusie suala la kodi kwa wafanyakazi
Mfanyakazi hasa wale wnaofanya sekta binafsi pindi wapatapo ka bonasi (sijui neno rasmi la kiswahili) basi serikali huchukua asilimia 30 ya hela yake je ni haki kwa serikali kuvuna kiasi chote hicho huku ikiwa haitoi huduma kwa jamii inavyostahili?
Friday, April 24, 2009
Habari zenu
Fahari yetu ina lengo la kuwapa wajasiriamali fursa ya kuonesha ubunifu wao na kuwapa uwanja mkubwa wa kutafuta masoko popote duniani. Ni fursa nzuri kwa yeyote apendae kujiendeleza ili kupata kile alichokusudia ili kumletea maendeleo.
Subscribe to:
Comments (Atom)

