Monday, April 27, 2009


Fahari yetu katika pitapita zake mitaani mwishoni mwa wiki ilivinjari Bagamoyo kusherehekea sikukuu ya muungano,ambayo kwa bahati mbaya mvua "ilivunja" muungano baada ya kumzuia rais wa Zanzibar mh. Dk. Karume kuudhuria sherehe hizo. Mvua hizo hazikuzuia mapumziko yetu ya sikukuu ampao tulijumuika na wananchi wengine,japo si wengi kutembelea mji ambao ni fahari yetu wa Bagamoyo, na kukuta mjasiliamali mmoja ambaye kwa sababu sikufanikiwa kuongea nae sitoweza kutaja jina ila nilipata fursa ya kupiga picha mojawapo ya vivutio vyake ambavyo vilinifanya nifurahie siku yangu na kujisikia furaha kuona kumbe kuna watanzania ambao ni wabunifu sana katika kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya Taifa letu kwani mbali na kuwaonesha watu fahari yetu hii,pia mjasiliamali huyu huuza mazao ya viumbe hawa nchi za nje na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.
HONGERA MDAU

No comments: